HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO
MTIHANI WA MOCK
DARASA LA VII
SOMO: URAIA NA MAADILI
1. Kama mtoto unayeishi katika nyumba yenye ukandamizaji wa kijinsia je ni hatua gani inaweza kutumika katika kutokomeza ukandamizaji wa kijinsia _____ A)Kutoa elimu kwa wote B) Kutoa elimu kwa wanaume C) Kutoa elimu kwa watu wazima D) Kutoa elimu kwa watoto E) Kutoa elimu kwa vijana
2.
Kitendo cha mtoto wa kike kumsimulia baba yake
jinsi anavyoepuka kushawishiwa kufanya ngono na kijana wa kiume kinaitwa_______
A) Kujijali B) Uaminifu C) Uwazi D) Nidhamu Binafsi E) Ustahimilivu
3.
Kama Mwanafunzi mwenye kujitolea katika
kufanya kazi mbalimbali za shuleni na jamii utatumia mbinu ipi kuwafanya
wanafunzi wenzako wajitolee kama wewe ______ A) Kuwashurutisha B) Kuwatumikisha
C) Kuwahamasisha
D) Kuwafuatilia E)Kuwaongoza
4.
Mojawapo ya vitendo si vya kawaida kwa mila na
desturi za mtanzania _____ A)Watoto Kuwaheshimu watu wazima B) Watoto
kuwakaripia watu wazima
C) Watoto kuwasaidia wazee kubeba mizigo
D) Watoto kuwaslimia watu wazima E) Kuishi vizuri na wanafamilia
5.
Wanawake na wanaume wanawajibu na majukumu
tofauti katika jamii. Ni neno gani linafafanua wajibu na majukuu hayo?______
A) Stadi B) Jinsia C) Jinsi D) Morali E) Usawa
6.
Mahusianao mabaya baina ya wanajamii yanaleta
matokeo hasi katika jamii zetu.Nini athari ya kunyanyapaa_____ A) Kukosekana
kwa amani na usalama
B) Kuimarika kwa upendo na urafiki C) Kuongezeka kwa umaskini na ujinga
D) Kuongezeka kwa migogoro na mapigano
E) Kukuza urafiki na uvumilivu
7.
Mkuu wa Shule ya Msingi Lemosho ameanzisha
kitendo cha ushauri nasaha katika shule yake. Nini umuhimu wa kitengo hicho ______A)
Kutoa muongozo wa jinsi ya kutatua changamoto B) Kueleza matatizo ya wanafunzi
hadharani
C) Kuwashauri wanafunzi wenye matatizo
kujieleza D) Kuwatangaza wanafunzi wenye matatizo E) Kuwatenge wanafunzi wenye
matatizo
8. Bwana mnyonge ni Afisa maendeleo wa kijiji cha Mlima ni ambaye huwaelimisha wanakijiji kuhusu majukumu ya kijamii. Ni jukumu lipi kati ya yafuatayo ni la kijamii:- _______ A) Kumwagilia bustani ya Familia B) Kufagia na kudeki nyumba C) Kusafisha chumba cha Kulala D) Kushiriki katika ujenzi wa Shule E) Kulisha Mifugo ya Nyumbani
9. Rasilimali za Taifa ni tunu zinazotakiwa kutunzwa na kuhifadhiwa nani ana wajibu wa kutunza na kuhifadhi _______ A) Maafisa wa Polisi B) Maafisa wa jeshi C) Raia wote D) Baba na Mama E) Viongozi wote wa serikali
10.
Kukubali
kukosolewa ni jambo la hekima sana. Onyesha sentensi sahihi kati ya hizi _______
A) Kukosolewa ni vibaya B) Tukubali kukosolewa tunapofanya makosa
C) Kukosolewa huleta ugomvi D) Anayekosea asikosolewe E) Tusikubali kukosolewa
11.
Kiongozi mmoja alikaa madarakani kwa muda
mrefu pasipo kuacha huku akijirimbikizia. Je hali ya kiongozi kujikusanyia
madaraka ya kila kitu huitwa?
_____ A) Uwazi B) Ukiritimba C) Umaskini D) Ujinga E) Utandawazi
12.
Chombo chenye mamlamka ya kumwondoa Rais madarakani
kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ______ A) Spika wa Bunge
B) Waziri Mkuu C) Mkuu wa Wilaya D) Mkuu wa Mkoa E) Wabunge
13. Jumuiya ya Afrika Mashariki awali ilikuwa na nchi au wanachama sita kabla ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kujiunga. Je nchi hii ilijiunga mwaka gani? ________ A) 1977 B) 2000 C) 2022 D) 2020 E)1967
14.
Mwenge wa Uhuru huitambulisha Tanzania kama
nchi huru. Ukiwa kama mtanzania unadhani huo mwenge uliwashwa na kupandishwa
katika mlima Kilimanjaro tarehe na mwaka gani?____ A) 26 April 1964 B) 9
December 1962
C) 8 Disemba 1961 D) 26 April 1962 e) 9 Disemba 1961
15.
Rais ndiye anayefanya uteuzi na kutengua viongozi
kati ya wafuatao yupi ambaye hateuliwi na Rais ________ A) Mawaziri B) Wakuu wa
Mikoa
C) Wakuu wa Wilaya D) Spika wa Bunge E) Mwanasheria Mkuu wa Serikali
16. Jeshi la Zimamoto lilianzishwa mwaka 2007,ukitaka kupata msaada wa jeshi hilo unapaswa kupiga simu namba ipi?____ A) 113 B) 114 C) 311 D) 511 E) 411
17.
Mama Sophia anapenda mwanae achangamane na
wenzake. Unafikiri lipi sio tendo la kumshirikisha mwanae na wenzake?______ A)
Kula B) Kucheza
C) Kusoma D) Kusaidiana E) Kubebwa na
mama yake
18. Kwanini watu wengi hupenda kutupa taka katika jaa_____ A) kuogopa muonekano B)kuogopa kuadhibiwa C) kuondoa uchafu katika mazingira D)kuogopa kukiuka mila na desturi E) kuogopa uzalendo
19.
Makosa ya Kimtandao yanakithiri siku hadi siku
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga sheria ya makosa ya mtandao
mwaka gani?_________
A) 2019 B)2020 C)2015 D)2010 E)2014
20. Kila mtu lazima awe mvumilivu ili kukabili changamoto kipi kati ya vifuatavyo siyo kitendo cha uvumulivu katika jamii_____ A) Kuwa na subira B) Kuwa jasiri na kuongea mbele za watu C) Kuomba na kutoa msamaha D) Kufuata sheria za kuwasilisha malalamiko E) Kutofanya migomo
21. Ili mipango iwe na ufanisi unapaswa kufuata hatua za utekelezaji mojawapo siyo faida ya kufuata hatua za utekelezaji wa mipango______ A) Kutambua rasilimali B) Kuongeza ufanisi C) Kutoa Rushwa D) Kujiamini E) Matumizi mazuri ya muda
22.
Mwanafunzi hufanya kazi zake kwa nadharia na
vitendo ili kuelewa zaidi, Je hutumia milango gani ya fahamu ili kufanikiwa _____
A) Pua na Mdomo
B) Milango yote ya fahamu C) Macho na
Ngozi D) Pua na Ulimi E) Ngozi na Midomo
23.
Haki za kibinadamu ni huduma anayopaswa
binadamu kupata kipi sio chombo cha utetezi sio chombo utetezi wa haki za
binadamu_____ A) Katiba ya Nchi
B) TAKUKURU C) Vyombo vya habari D) Tume
ya haki za Binadamu
E) Bunge la Tanzania
24. Kukua kwa Utandawazi katika jamii yoyote huwa na manufaa na madhara yake. Nini madhara ya Utandawazi katika jamii______ A) Kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili B) Kudumaa kwa teknolojia ya habari C) Kupungua kwa mwingiliano wa watu D) Kupungua kwa fursa za ajira E) Kudumishwa kwa huduma za jamii
25.
Ni kwa namna gani mafundisho ya kijamii
husaidia kutawala hisia mbaya na mihemko kwa vijana _______ A) Hisisitiza
amani, Upendo na Kusameheana
B) Hujenga, matatizo chanya katika kutatua changamoto C)Husisitiza kufanya
mazoezi ya mwili na akili D) Husisitiza kushiriki katika kutatua matatizo ya
wengine E) Husaidia kutafuta taarifa juu ya matatizo ya jamii
26. Kiongozi Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni ni Waziri Mkuu. Ipi kati ya zifuatazo ni sifa ya Waziri Mkuu ______ A) Lazima awe Msomi B) Lazima awe Mwanaume C) Lazima awe Mbunge D) Lazima awe Mwana CCM E) Lazima achaguliwe na Wananchi
27.
Zifuatazo ni vitendo ambavyo vinalenga kulinda uhuru na umoja wa kitaifa isipokuwa
_____ A) kuheshimu sheria za nchi B) kulinda mipaka ya nchi
C) kuheshimu haki za binadamu D) kuondoa matendo maovu E)kuheshimu viongozi
28. Ipi kati ya zifuatazo si faida za kubuni njia mbadala katika kukabiliana na tatizo:-______A) Husaidia kutatua changamoto iliyoshindikana B) Husaidia kutatua tatizo lililokosa ufumbuzi C) Husaidia kupata utatuzi wa tatizo jipya D)Husaidia kupata muda wa ziada wa kujifurahisha na kujitafakari E) Kuweza kusaidia kufika malengo
29. Malengo ni dhamira au kusudio la kutelekeza jambo lililopangwa. Je, kuna aina kuu ngapi za malengo_____ A) Tatu B) Mbili C) Nne D) Tano E) Moja
30.
Mambo yote lazima yafanyike kwa utaratibu
maalumu. Je, mambo yanayopaswa kukamilika kabla ya mengine hujulikana kama________
A) Mwanzoni B) Vipanyuma C)Muktadha D)
Vipaumbele E) Ving’ang’anishi
31. Mtu mnafiki lazima asiruhusiwe kuiongoza jamii. Utamtambuaje mnafiki katika jamii ______ A) Huchonganisha watu B) Husema kweli C) Huwa na uhakika na ayasemayo D) Anawachonganisha watu E) Anapenda suluhu
32.
Watu wote wanapaswa kuheshimiana na kusaidiana.
Kipi kati ya vifuatavyo ni kitendo cha kuharibu uhusiano baina ya watu______ A)
Kutothamini wengine
B) Kuwaonya wengine C) Kufanya kazi kwa bidii D) Kusema Ukweli
E) Kusaidiana
33.
Nchini Tanzania kila baada ya miaka kumi
hufanyika zoezi la Sensa la uhesabuji wa watu na makazi. Je mwaka huu sensa hufanyika
tarehe ngapi?______
A) 23 Agosti 2022 B) 27 Agosti 2022 C)
20 Octoba 2020 D) 23 Julai 2021 E) 29 October 2022
34. Mihimili
ya dola hutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya Tanzania. Je, Askari
polisi alimpiga Raia na kumuua bila kukusudia shauri lake litaamuliwa na muhimili upi wa dola ______ A) Baraza la Mawaziri B) Bunge
C) Serikali D) Mahakamani E) Katiba ya Tanzania
35. Elimu ya afya ya Uzazi ni muhimi kwa manufaa ya watoto wetu. Elimu hiyo inahusisha vitu vifuatavyo isipokuwa______ A) Ujauzito B)Ukuaji na Kubalehe C) Magonjwa ya Mlipuko D) Masuala ya Hedhi E) Uzazi wa mpango
36. Mali za
umma lazima zitunze kwa manufaa ya watanzania. Kipi kati ya vifuatavyo si
kitendo cha matumizi ya mali za umma _____A) Rushwa
B) Ufisadi C) Mikataba mibovu D) Kutojali
mali za umma E) Kuchagua viongozi kwa kupiga kura
37. Uhusiano mzuri katika jamii huleta amani na utulivu.
Ni kipi kati ya vifuatavyo kinadumisha uhusiano mzuri baina ya watu wenye
tamaduni tofauti_____
A) Kusalimiana B) Aina ya mavazi C) Aina ya Chakula D) Matumizi ya Lugha E)
Shughuli za kiuchumi
38. Kwa sheria tume ya Uchaguzi Tanzania mgombea kwa nafasi ya uraisi ni lazima awe na umri usiopungua miaka ____A) 21 B) 31 C) 40 D) 41 E) 45
39. Mikakati gani ifanyike ili kuzuia watu wenye tabia ya
kuharibu uhusiano mzuri baina ya watu?____ A) Kuwaelimisha umuhimu wa umbea B)
Kuwaelimisha juu ya Uongo na Umbea C) Kujenga uelewa juu ya Kuepuka wivu na
kusengenya D) Kujenga uelewa juu ya kutokuwa huru kusema uongo
E) Kujenga uelewa juu ya wajibu wa kuigiza na kusengenya
40. Meya wa halmashauri huchaguliwa kutoka kwenye kundi fulani la watu. Je kundi hilo ni _______ A) Wabunge B) Madiwani C) Mawaziri D) Wakuu wa Wilaya E) Wananchi
SEHEMU: B (ALAMA 10)
Katika swali la 41 – 45 andika majibu sahihi katika nafasi zilizoachwa wazi kwenye fomu ya kujibia uliyopewa (OMR) kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi
41. Chombo chenye mamlaka ya kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ________________________
42. Vitu muhimu na vya thamani vinavyomilikiwa na mtu shirika, au Serikali hujulikana kama ___________________
43. Katika jamii zetu baadhi ya mila huathiri sana wanawake, mojawapo ya mila hizi ni ukeketaji. Eleza madhara mawili yanayotokana na ukeketaji wa wanawake __________________
44. Wahitimu wa darasa la saba walisoma somo la uraia na maadili wanawezaje kuinufaisha jamii zao kwa elimu hiyo waliyoipata_____________________
45. Eleza faida zozote mbili za serikali ya Kidemodrasia___________________